VISUMBUFU VYA MAZAO SHAMBANI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year1980
Mazao yaliyo shambani ni viumbe hai. Yakishambuliwa na
visumbufu huweza kudhoofika au kufa kabisa. Iwapo
hayatakufa, mavuno yatakayopatikana yatakuwa kidogo. Ubora
na thamani ya mavuno hayo pia hupungua. Matokeo ya hali hiyo
ni hasara kubwa kwa mkulima, taifa na wote wanaotegemea
mazao hayo. Hasara hiyo inaweza kuwa ni njaa kwa familia ya
mkulima au kukosa fedha. Kwa taifa , hii inaweza kuwa ni njaa
kwa taifa zima au ukosefu wa fedha za kigeni na viwanda
vinavyotumia mazao hayo kukosa malighafi.
Pay with DPO