USTAWISHAJI BORA WA CHAI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2004
Chai ni moja ya mazao muhimu nchini. Zao hili hustawishwa kwa ajili ya majani yake ambayo yana asilimia 4 ya kafeini.
Kwa mkulima, ni zao ambalo huweza kumpatia fedha kila wiki kwa kuchuma majani mabichi na kuyauza. Kwa taifa,
chai huuzwa nchi za nje na kuingiza fedha za kigeni. Hili ni moja ya mazao muhimu ambayo huingiza kwa wingi fedha za kigeni.
Chai ni kinywaji kizuri kwa wananchi. Kinachangamsha na kufurahisha wanywaji. Hakileweshi kama pombe.
Kwa sababu hii unywaji wake husaidia kupunguza ajali na madhara mengine yaletwayo na vileo.
Pamoja na umuhimu wa zao hili, bado wapo wakulima wengi, hasa wale wadogo,
ambao hawaelewi vizuri kanuni za kilimo bora cha zao hili. Pamoja na kueleza mambo mengine muhimu yanayohusu chai,
kitabu hiki kitawafundisha wasomaji historia ya zao hili, umuhimu wake na jinsi ya kulistawisha, kulitunza, kulichuma,
kuuza majani mabichi ya chai na kadhalika.
Pay with DPO