Ufafanuzi wa Sheria ya Kumiliki Ardhi Vijijini Tanzania
-
AuthorAl-Muswadiku K. Chamani
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
Ardhi ni rasilimali kuu na msingi mkubwa wa maendeleo ya wakazi wa
Vijijini na Mjini. Ustawishaji wa mazao na ufugaji wa aina mbalimbali
wa viumbe hai hufanyika kwenye ardhi. Aidha, majengo yote
na miundombinu ya aina mbalimbali hujengwa kwenye ardhi. Kwa hiyo,
ardhi ni chanzo kikuu cha uhai na maendeleo ya binadamu. Kutomiliki
ardhi ni hasara, maana hatimaye huwezi kuwa na mali isiyohamishika
kama vile nyumba au majengo wala shamba la mazao au la mifugo.
Kwa Tanzania, ardhi yote iliyo ndani ya mipaka ya nchi, iko mikononi
mwa Rais wa nchi, anaisimamia kwa niaba na kwa faida ya Watanzania
wote waliopo na watakaozaliwa baadaye.
Pay with DPO