Tusiwahukumu Changudoa
-
AuthorJames B. Kalugira
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2016
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Changudoa ni “mwanamke anayezunguka mitaani usiku ili kujiuza kwa wanaume kwa ajili ya kupata fedha.” Wanawake hawa hawapendi kazi hii ya kuuza miili yao bali ni shida tu zimewalazimisha kufanya kzi hii, baada ya kukosa kazi nyingine. Katika nchi hii wanaitwa majina mbalimbali kama vile, Malaya, wahuni, watenda dhambi n.k. Wao wenyewe wanasikitishwa na jamii kuwaona hivyo na kuwahukumu hivyo. Kwao, hii ni kazi inayowawezesha kuisha na kupata mahitaji yao ya lazima.
Wanawake hawa kutokana na kuzidiwa na hali ya maisha wanatamani kupata, lakini, kazi hazipatikani, maana ili kupata kazi unatakiwa kujuana na watu, lakini, dada hao hawana watu wa kuwasaidia kupata kazi, hawana pesa za kuhonga kupata kazi. Wanatamani kuolewa ili kuwa na familia zao, kuwa na watoto wao, kuitwa mama fulani au kuitwa yule mama mume wake ni fulani, ndoto zao zinafifia kidogokidogo, matarajio yao ya kuolewa na kutunza familia yanaishia kwenye mateso makali kama ya kuchomwa na mwiba! Matarajio na ndoto zao nzuri zinazimwa.
Katika kitabu hiki, mwandishi ametumia kalamu yake kujenga hoja ya kuwatetea changudoa dhidi ya kuhudumiwa bila kusikilizwa na kutoa mwito kwa kila mmoja, kwenye nafasi yake aweze kuwasaidia ili kutokana na adha hii. Aidha, mwandishi anaamini kuwa, kila mtu anaweza kubadilisha tabia na mwonekano kwenye jamii endapo atasikilizwa na kuwezeshwa kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea kama vile, Marekani anakoishi na kufanyakazi mwandishi
Pay with DPO