Rita Koku

Rita Koku

4.0
  • AuthorMaria Ruhumuliza Paulo
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2023

Rita Koku ni msichana mzuri mwenye umbo la kupendeza na pia alikuwa na tabia nzuri. Alikuwa ni kifungua mimba katika familia ya Bwana na Bibi Philipo. Kutokana na tabia yake nzuri wazazi wake walimpenda sana. Alifanikiwa kusoma hadi kidato cha nne na kupata sifa za kuweza 
kujiunga na chuo cha ualimu.
Lakini, Rita hakupenda kwenda Chuo hicho. Wazazi wake walimshawishi aende Chuoni ila Rita hakukubaliana nao. Wazazi wake walimkabidhi biashara ya Duka la Rejareja. Akiwa dukani hapo vijana wa aina mbalimbali walitumia nafasi hii kumtafuta Rita kimapenzi. Rita hakuwa msichana 
mwenye papara, hivyo, hakupenda kujirahisi kwa wanaume hao. 
Baadaye Rita aliamua kupendana na kijana aitwaye Leonard, kwa kifupi Lenny. Hatimaye, Lenny alimweleza Rita kwamba alitaka amuoe. 
Baada ya Rita kufikiri kwa siku kadhaa alimkubalia. Walipima UKIMWI na kukutwa hawana virusi vya ugonjwa huo. Rita alimweleza mama yake habari za kumpata mchumba. Lakini, mama yake hakukubaliana naye kwa sababu wazazi hawa walishamwandalia Rita mvulana wa kumuoa ambaye alikuwa bado yuko masomoni.
Lakini, Rita alijichukulia uamuzi, akaolewa na Lenny baada ya kutoroshwa nyumbani kwao. Huko, Lenny hakutaka Rita atembelee majirani. Rita akiwa mjamzito, Lenny alipata safari na Rita alitumia muda huo kwenda kwa jirani yake Bi Amina ambaye alimjulisha kuwa Lenny alikuwa jambazi sugu.
Ni nini kilimpata Rita ambaye anapata habari hizi akiwa mjamzito? Je, wazazi wa Rita wana hali gani baada ya Rita kutoroshwa nyumbani?
Soma hadithi hii ya kusisimua uyajue haya.

Pay with DPO

dpo
Book Title Rita Koku
Author Maria Ruhumuliza Paulo
ISBN 978-9987-426-29-4
Edition Language
Date Published 2023-09-15
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 58
Chapters 9

Related Books

Penzi liliponzwa
Penzi liliponzwa
  • RIWAYA
Tzs5,000.00 Tzs10,000.00
View
Tusiwahukumu Changudoa
Tusiwahukumu Changudoa
  • RIWAYA
Tzs5,000.00 Tzs10,000.00
View