SAYANSI YA MIMEA YA MAZAO

SAYANSI YA MIMEA YA MAZAO

4.0
  • AuthorPius B. Ngeze
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2003

Duniani kuna viumbe vya aina mbili. Aina ya kwanza ni viumbe
visivyo na uhai, kwa mfano, hewa na mawe. Aina ya pili ni viumbe vyenye
uhai. Viumbehai navyo vinaweza kutengwa katika makundi mawili, yaani
mimea na wanyama. Mimea na wanyama hutegemeana. Chakula kikuu cha
wanyama ni mimea mbalimbali pamoja na mazao yatokanayo na mimea.
Kwa hiyo, tunaona kwamba wanyama hutegemea mimea kwa chakula.
Bila mimea wanyama wote muhimu watatoweka duniani. Kwa upande
mwingine, kinyesi cha wanyama pamoja na mabaki kadhaa yanayopatikana
wakati wakifa au kuchinjwa hutengeneza mboji ambayo ni chakula bora
cha mimea. Mboji hiyo vilevile ni ya manufaa makubwa kwa udongo
pamoja na viumbe vingine vii shivyo undongoni. Viumbe hivi huiwezesha
mimea kustawi zaidi. Kwa hiyo, tunaweza kusema pia kwamba mimea
hutegemea wanyama kwa mahitaji yake ya chakula.

Pay with DPO

dpo
Book Title SAYANSI YA MIMEA YA MAZAO
Author Pius B. Ngeze
ISBN 978-9987-671-38-0
Edition Language Kiswahili
Date Published 2002-01-23
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 76
Chapters 6

Related Books

Banana and their Management
Banana and their Management
  • KILIMO CHA MAZAO (MORDEN CROPS HUSBANDRY)
Tzs4,000.00 Tzs4,500.00
View
COTTON IN TANZANIA: Breaking the Jinx
COTTON IN TANZANIA: Breaking the Jinx
  • KILIMO CHA MAZAO (MORDEN CROPS HUSBANDRY)
Tzs4,000.00 Tzs4,500.00
View