Pius Bakengera Ngeze Maisha yake na Baada ya Miaka 70
-
AuthorPadri Privatus Karugendo
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2013
Kitabu hiki kimeundwa na sura kumi na moja (11). Sura ya
kwanza inahusu kumbukizi ya miaka 70 ya kuzaliwa kwake na
ina maelezo ya mke wake, mama Rachel Wizeye Mbonimana,
juu ya ‘anavyomfahamu mumewe’.
Sura ya pili ina maoni ya watoto wake watano: Catherine
Balankunda akiwa Marekani, William Niyongoma akiwa Juba,
Sudani ya Kusini, Fides Shimilimana akiwa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Flavia Niyikiza akiwa TRA Mbeya na Mariapia
Niyimbona akiwa Chuo Kikuu cha Mzumbe. Kila mmoja anaeleza
anavyomfahamu baba yake. Ninaamini Mzee Ngeze atafurahi
kusoma sura hiyo na kujua anavyoeleweka kwa wanaye. Nao
pia watafurahi kusoma wanavyomwelewa baba yao.
Sura ya tatu ina maelezo ya Watanzania wengine kumi na
watatu kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu wakieleza
wanavyomfahamu. Wale waliokuwa hawamwelewi vizuri Mzee
Ngeze, sasa watamjua zaidi kwa kusoma sura hii. Hata mimi
nilikuwa simfahamu kwa kiasi hicho!
Pay with DPO