Maisha na Ujasiri wa Mjane
-
AuthorTheophilda Tinkasimire Tikawa
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2015
Bibi Theophilda Tinkasimire Tikawa, mwandishi wa kitabu
hiki kinachosimulia maisha yake tangu kuzaliwa, kukua,
kusoma shule, kuolewa, kuajiriwa, kufiwa na mume na hatimaye
kufiwa na wazazi wake, ni mama mjane jasiri, mcha Mungu,
mpambanaji, mpenda maendeleo na Mwalimu aliyependa
sana watoto nchini wapate elimu. Ipo mifano hai ya watoto
aliowasaidia na kuwahimiza wasome kwa uwezo wao wote
na sasa ni Maprofesa na Madaktari. Kitabu hiki kinaongelea
safari ya kishujaa ya maisha ya Mwalimu Theophilda ambaye
kwangu binafsi amekuwa mfano wa wanawake wasiokubali
kubweteka na badala yake kujisimamia, kuweka malengo na
mikakati ya maisha na kuisimamia kijasiri licha ya changamoto
mbalimbali hasa za unyanyaswaji wa kijinsia zinazowakabili
akina mama na, hasa, wajane, na waliozaliwa katika mazingira
magumu yaliyojaa mila na desturi za kuwanyanyapaa watoto
wa kike.
Mwalimu Theophilda aliwapenda na kuwaheshimu wazazi
wake wote. Alikuwa na baba wawili: baba mzazi na baba mlezi
aliyempata kwa mujibu wa mila na tamaduni za kabila lake
kama utakavyogundua ukisoma kitabu hiki. Kuolewa kwa
Bi. Theophilda akiwa na umri mdogo na baadaye kufiwa na
mume mapema akiwa na umri mdogo wa miaka 37 lilikuwa
pigo kubwa kwake, lakini, kwa ushupavu wake na msimamo
mkali aliamua kutoolewa tena na kuwalea watoto wake
Bruno, Felix, Letisia na Victor ambao walikuwa bado wadogo.
Pay with DPO