NGUZO ZA KILIMO
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2004
Kitabu hiki kinahusu nguzo za kilimo. Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu, neno „nguzo” limeelezwa kwamba ni “1. muhimili wa kutengenezea mapaa ya nyumba; miti iliyosimama wima kwenye viambaza vya nyumba. 2. tegemezo; msingi; kwa mfano, nguzo za dini.” Tumezoea kusikia au kuona nguzo za nyumba. Wajenzi wa nyumba na majumba makubwa wanaelewa sana maana ya nguzo na umuhimu wake katika kuifanya nyumba inayojengwa iwe imara. Nyumba hizo zinaweza kuwa za miti au za vyuma na mchanganyiko wa saruji, mchanga na maji. Nguzo ni nguzo. Tofauti inaweza kuwa tu katika ugumu au uvumilivu wa kubeba uzito. Lakini, umuhimu ni uleule. Yaani, wa kuifanya nyumba hiyo iwe imara, ipendeze na idumu miaka mingi sana. Kwa hiyo, nguzo za kilimo zinaweza kufananishwa na nguzo za nyumba zilizoelezwa hivi punde. Nguzo za kilimo ni yale mambo ambayo bila kutambuliwa na kuzingatiwa hakuna kilimo, na hasa, hakuna maendeleo ya kilimo yatakayopati-kana. Lakini, uzingatiaji wake katika jitihada zetu za kuendeleza kilimo unaweza kuleta mapinduzi makubwa katika kilimo chetu.
Pay with DPO