MWONGOZO WA UHASIBU WA SHAMBA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2003
Katika kitabu hiki, neno ‘shamba’ limetumika likiwa na
maana ya eneo la ardhi ambamo shughuli mbalimbali za
kilimo, yaani, ustawishaji wa mimea ya mazao na malisho ya
mifugo na ufugaji wa aina mbalimbali za wanyama, ndege na
upandaji wa miti huweza kufanyika. Neno ‘kilimo’ lina maana
ya ustawishaji wa mimea ya mazao, malisho ya mifugo,
ufugaji na upandaji wa miti. Neno ‘mkulima’ lina maana
ya mtu anayefanya shughuli za kilimo.
Ndani ya kitabu hiki, aina ya fedha iliyotumika inaitwa
‘pesa.’ Pesa moja ina senti 100. Yaani, senti 100 ni sawa
na pesa moja. Nimetumia “pesa” ili kuwarahisishia
wasomaji kuelewa yaliyomo kitabuni. Hata hivyo, msomaji
ana uhuru wa kutumia aina nyingine ya fedha badala ya
pesa, mradi kufanya hivyo, ni kwa faida yake au ni kufanya
somo lieleweke kwa urahisi.
Pay with DPO