Mwongozo wa Kilimobiashara cha Parachichi
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2023
Mwongozo wa Kilimobiashara cha Parachichi
Parachichi, kama zao la biashara, ni jipya nchini. Ni zao lenye faida ya kilishe,kiafya, kimatibabu na kiuchumi. Uzalishaji wake bado uko chini ukilinganisha na nchi moja jirani. Hata hivyo, kwa sasa paraachichi ni mojawapo ya mazao machache yaliyoteuliwa na serikali kuwa ya mkakati. Ni zao la biashara ambalo sasa linahamasishwa listawishwe kibiashara na wakulima wa mashamba madogo na makubwa. Hapa nchini hustawishwa aina kadhaa za parachichi, lakini, zilizo muhimu kibiashara kwa sasa ni mbili, yaani, Hass na Fuerte. Lakini, kipaumbele ni kwa Hass ambayo ina sifa zote za kuuzwa nchi za nje. Bei yake ni kubwa sana ndani na nje ya nchi. Kwa sababu hii, wakulima wengi wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kupanda miche kwa kutegemea uwezo wa mkulima na upatikanaji wa ardhi yenye afya na mazingira yanayotakiwa ya kuistawisha kibiashara.
Katika kitabu hiki, mwandishi Pius B. Ngeze ameeleza kanuni za kuistawisha kibiashara. Anashauri mkulima aanze na idadi ndogo ya miche kati ya 20-100. Mimea 100 ni sawa na eka moja. Mtu asikimbilie kuanzisha shamba kubwa kama hakujipanga vizuri kwa mtaji na utaalamu wa kuliendesha.
Mwisho mwa kitabu ipo Sura inayoonyesha gharama za kuanzisha na kutunza shamba la parachichi la eka moja na Uchambuzi wa faida/hasara kwa kipindi cha hadi miaka kumi (10) ya kwanza.
Kitabu hiki kitakuwa cha marejeo kwa wakulima, maofisa ugani na viongozi wa wananchi na wakulima wa ngazi mbalimbali.
Pay with DPO