Mwongozo wa Kilimobiashara cha Mipapai

Mwongozo wa Kilimobiashara cha Mipapai

4.0
  • AuthorPius B. Ngeze
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2022

Kitabu kinaeleza Sayansi ya Muundo wa Mpapai; Faida zake; Aina bora na Maumbo ya Mapapai; Mifumo ya kilimo cha Mipapai; Mahitaji makuu ili iweze kustawi vizuri; Maandalizi ya Miche; Maandalizi ya Shamba na Mashimo; Wakati unaofaa kuhamisha miche kutoka kitaluni na Upandikizaji shambani; Utunzaji wa Mimea shambani;

Aina na kiasi cha mbolea kinachohitajika kustawisha mmea. Sababu za Maua na Mapapai machanga kudondoka kutoka kwenye Mpapai;

Visumbufu vya mipapai na Udhibiti wake; Upevukaji; Uvunaji na huduma zitolewazo baada ya kuvuna; Gharama za kuanzisha shamba la eka moja na Mapato kutokana na eka hiyo na Utunzaji

wa Kumbukumbu za shughuli za Shamba. Ili mkulima aweze kufanikisha kilimo cha mipapai kusudi avune

mapapai mengi na yaliyo bora ili kuyauza na kujipatia mamilioni ya shilingi, lazima ajiandae vizuri na awe na mtaji wa kutosha kwa ajili ya:

  • Upatikanaji na umiliki wa ardhi ya kupanda mipapai.
  • Utayarishaji wa shamba na mashimo.
  • Ununuzi wa mbegu bora na maandalizi ya miche.
  • Upandikizaji wa miche shambani na utunzaji wa shamba.
  • Ununuzi wa mbolea za asili na mbolea za viwandani.
  •  Ununuzi wa viuatilifu vya kudhibiti magonjwa na wadudu.
  • Upatikanaji wa chanzo cha kudumu cha maji kwa ajili ya umwagiliaji mvua zikikatika.xii
  •  Kulipia vibarua na wafanyakazi wa kutunza shamba, kunyunyizia mimea viuatilifu kila baada ya siku saba (7) wakati wa mvua na siku 14 wakati wa kiangazi, kuvuna, kutayarisha mavuno, kuuza n.k.

Gharama za Kuanzisha na Kutunza shamba la eka moja na Ukokotoaji wa Mapato kutokana na eka hiyo zimeonyeshwa katika Sura ya 22.

Kwa hakika, hiki ni kitabu cha lazima kwa wakulima wa zamani na

wapya, maofisa ugani, viongozi, na mameneja wa mashamba.

Pay with DPO

dpo
Book Title Mwongozo wa Kilimobiashara cha Mipapai
Author Pius B. Ngeze
ISBN 978-9987-07-083-1
Edition Language
Date Published 2023-09-07
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 129
Chapters 23

Related Books

Banana and their Management
Banana and their Management
  • KILIMO CHA MAZAO (MORDEN CROPS HUSBANDRY)
Tzs5,000.00 Tzs20,000.00
View
COTTON IN TANZANIA: Breaking the Jinx
COTTON IN TANZANIA: Breaking the Jinx
  • KILIMO CHA MAZAO (MORDEN CROPS HUSBANDRY)
Tzs5,000.00 Tzs20,000.00
View