Mwongozo wa Kilimo Bora cha Alizeti
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2007
Alizeti ni zao linaloweza kuwakomboa wakulima kiuchumi. Pia,
huchangia pato la taifa na kuliingizia taifa fedha za kigeni kwa kuuza
bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kutokana na mbegu zake.
Wajibu wa wakulima ni kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kanuni
za kilimo bora cha alizeti, ambazo ni pamoja na hizi zifuatazo
ambazo zimefafanuliwa kitabuni:
1. Kutayarisha vizuri shamba.
2. Kila msimu kununua mbegu chotara za kupanda kutoka kwenye
maduka yanayouza pembejeo za kilimo yaliyoidhinishwa na
serikali.
3. Kupanda mbegu hizo kwa nafasi inayopendekezwa na
wataalamu.
4. Kuchagua vizuri muda wa kupanda. Muda mzuri ni ule ambao
utafanya alizeti itoe maua wakati kukiwa na mvua na wakati wa
kukomaa kuwe na hali ya ukame.
Pay with DPO