MWONGOZO WA HIFADHI BORA YA NAFAKA NA JAMII YA MAHARAGE
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2021
Lengo la mkulima kustawisha mimea ya mazao ni hatimaye apate
mavuno mengi na yaliyo bora. Wingi wa mavuno unamaanisha uzito.
Uzito hupimwa kwa kilogramu. Kwa upande mwingine, ubora wa
mavuno huonekana kwa rangi yake ya asili, ladha, harufu na uwezo
wa mbegu kuota na iwapo mbegu hazina dalili za magonjwa au
kuliwa na panya, ndege n.k.
Wakulima wengi hukosa au hupoteza vyote viwili, yaani, mavuno
hupungua uzito na ubora pia hupungua. Inakadiriwa kuwa,
asilimia ishirini na tano (25%) ya uzito wa mavuno yaliyotegemewa
na wakulima, hupotea kwa njia mbalimbali ambazo zimeelezwa
kitabuni. Kiasi hicho cha upotevu ni hasara kubwa kwa wakulima
husika na taifa. Aidha, ubora wa mavuno hushuka sana na mkulima
kuzidi kudidimia kimapato.
Pay with DPO