MWONGOZO KWA WAANDISHI WA HABARI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2004
Mnamo tarehe 23 – 30 Agosti, 1991 kilichokuwa Chama cha Ushirika cha Waandishi na Wachapishaji cha Kagera (Kagera Writers and Publishers Co-operative Society Ltd) kiliandaa Warsha Mjini Bukoba kwa ajili ya Waandishi wa Habari kutoka Vijijini wa gazeti lililoitwa wakati huo, Kagera Leo. Baada ya kumalizika Warsha hiyo, makala na kumbukumbu za majadiliano ya washiriki wa Warsha hiyo, zilichapishwa kitabu. Kitabu hicho kiliitwa Mwongozo kwa Waandishi wa Habari Vijijini kikiwa na ISBN 997 6 982 08 9. Wataalamu na mabingwa kati-ka fani ya uandishi wa habari walialikwa kutayarisha ma-kala na kuziwasilisha kwenye Warsha hiyo na walifanya hivyo.
Chama hicho “kilikufa” tarehe 25 Februari, 1997 kutokana na Azimio la Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Cha-ma hicho. Ingawa Chama hicho kimekufa, lakini maudhui na umuhimu wa baadhi ya makala zilizowasilishwa kwenye Warsha hiyo bado ni mazuri hadi sasa, maana ukweli haufi. Ni kwa sababu hii, tumeamua kuchapisha baadhi ya makala na kutoa toleo jipya la kitabu hicho kwa jina jipya la Mwongozo kwa Waandishi wa Habari.
Pay with DPO