MISITU NA HIFADHI YA MAZINGIRA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2003
Neno ‘mazingira’ lina maana ya vitu vyote vilivyo hai na visivyo
hai vinavyomzunguka binadamu. Mazingira ni pamoja na
maliasili zinazopatikana kwenye maeneo tunayoishi. Sera ya
Taifa ya Mazingira inaeleza kuwa neno ‘mazingira’ “linajumlisha
hewa, ardhi na maji, uhai wa mimea na wanyama ukiwamo uhai
wa binadamu; hali ya kijamii, kiuchumi na hali inayoshawishi
maisha ya kijamii, kiuchumi na hali inayoshawishi maisha ya
wanadamu na jumuia zao; majengo, miundombinu, mashine na
mambo mengine yaliyoundwa au kutengenezwa na mwanadamu,
maada ngumu, vimiminika, gesi, harufu, joto, sauti, mtetemo
au mnururisho unaotokana moja kwa moja au matokeo ya
shughuli za mwanadamu; pamoja na, ama sehemu moja au
mchanganyiko wa uhusiano wa vyote vilivyotajwa hapo juu.”
Pay with DPO