MISINGI YA KILIMO BORA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year1976
Mojawapo ya matatizo ambayo yanakabili juhudi zetu za kuendeleza
uchumi na maisha yetu ni ukosefu wa vitabu vya kutosha vilivyoandikwa
katika lugha ya Kiswahili juu ya shughuli zetu muhimu za kiuchumi.
Katika nchi hii zaidi ya asilimia tisini ya watu hutegemea kilimo kwa
uchumi na chakula chao. Kwa hiyo, kilimo ndio msingi mkuu wa
maendeleo ya uchumi wa wananchi na taifa zima.
Kadhalika, kiasi kikubwa cha mapato ya serikali hutokana na kilimo.
Licha ya mapato ya fedha ambayo serikali na wananchi wanapata kwa
kuuza mazao ya kilimo nchini, taifa halina budi kuuza mazao ya kilimo
zaidi katika nchi za nje ili tupate fedha za kigeni ambazo zinahitajika
kutuwezesha kununua vyombo vya kuzalisha mali zaidi ambavyo kwa
wakati huu hatutengenezi wenyewe. Vyomo hivi ni kama vile matrekta
ambayo yanasaidia wananchi kulima mashamba makubwa na kuongeza
mavuno na mapato.
Pay with DPO