MIGOMBA UANZISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year1991
Mwandishi wa kitabu hiki, akiwa mtaalamu wa kilimo, anaeleza jinsi ya kuanzisha na kutunza shamba la migomba. Kilimo cha kisasa cha migomba siyo rahisi kama inavyofikiriwa, kwani ukilima ovyo shamba lako na bila kulitunza vizuri huwezi kupata mavuno ya kuridhisha. Kwa hiyo, jitihada na utafiti wa mwandishi wa kuweza kuandika kitabu hiki unahitaji pongezi na kupewa moyo zaidi wa kuzidi kuandika. Chipukizi lililochaguliwa ndilo hupandwa. Baada ya kupandwa huota na kuendelea kukua. Baada ya miezi tisa mgomba hutoa ndizi. Miezi mitatu hadi minne baadaye ndizi hukomaa.
Ndizi ni chakula kikuu hapa nchini.Wananchi wa mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya hulithamini sana zao la ndizi. Kuna ndizi za aina nyingi, lakini zipo aina kuu nne: (a) ndizi za kupika, (b) ndizi za kutengeneza pombe, (c) ndizi zinazoliwa baada ya kuiva, (d) ndizi za kuchoma au kukaanga. Hata hivyo, bado aina kuu hizo zinaweza kugawanyika zaidi. Kwa mfano, ndizi zinazostawishwa katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambazo huwa ni za pombe (hutengenezwa pombe iitwayo mbege); haziwezi kutumika kutengeneza pombe ya lubisi inayonywewa na wakazi wa mkoa wa Kagera. Lakini baadhi ya ndizi za Kagera zinaweza kutengeneza mbege. Kadhalika kuna ndizi laini na ndizi ngumu wakati wa kula. Matoke kutoka Kagera huwa laini sana na mshare kutoka Arusha na Kilimanjaro huwa ngumu. Kila aina ina sifa zake wakati wa kula licha ya ulaini au ugumu wake.
Pay with DPO