Malisho ya Mifugo
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
Mifugo bila kupewa au kujipatia chakula haiwezi kuishi. Chakula ni muhimu kwa mifugo kama ilivyo kwa binadamu. Chakula kikuu cha mifugo ni malisho. Malisho ni mimea ya aina mbalimbali, kama vile, nyasi na mimea ya mazao ya foreji. Hii ni pamoja na mikundekunde na miti. Asilimia 75-80 ya chakula cha mifugo ni malisho na asilimia iliyosalia ni vyakula vya ziada. Kwa wafugaji wadogo ambao ndio wengi hapa nchini, malisho ndicho chakula pekee cha mifugo yao. Lakini, malisho hayo ni hafifu, maana hayana viinilishe muhimu vinavyotakiwa na kwa kiasi kinachotakiwa. Vii nilishe hivyo ni wanga protini, mafuta, madini na vitamini. Matokeo yake ni kuwa afya yake (mifugo) si ya kuridhisha na uzalishaji wa nyama, maziwa n.k. uko chini. Hii inajidhihirisha kwa jinsi mifugo ilivyokonda na idadi ya vifo kila mwaka, hasa kipindi cha ukame.
Pay with DPO