Mahitaji ya Maji ya Kustawisha Miembe na Umuhimu wa Umwagiliaji
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2022
Maji ni pembejeo namba moja kwa kilimobiashara. Bila maji hakuna uhai duniani. Bila maji hakuna kustawisha mazao ya mimea. Bila maji ufugaji wa aina yoyote hauwezekani. Hakuna lolote linaweza kufanyika bila matumizi ya maji.
Katika nyakati hizi ambapo kutokana na mabadiliko ya tabianchi majira ya mvua tuliyoyazoea hayaaminiki tena, upatikanaji wa maji kwa njia ya Umwagiliaji wa miembe ni wa lazima sasa kuliko ilivyowahi kuwa huko nyuma. Na ili uweze kupata maji ya kumwagilia shamba la miembe, lazima kuwa na chanzo cha maji kinachoaminika na cha kudumu.
Kitabu hiki kinaeleza kwa muhtasari, kazi na faida za maji kwa miembe na namna bora ya kuyatumia kunyweshea (miembe). Aidha, kinaeleza kuhusu umwagiliaji na aina za vyanzo vya maji ya kumwagilia. Ni muhimu kila mkulima awe na elimu iliyomo kitabuni kwa
mafanikio ya kilimo cha miembe.
Pay with DPO