MAGONJWA NA WADUDU WA MIPAPAI NA MAPAPAI NA UDHIBITI WAKE
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2023
Magonjwa na wadudu ni visumbufu vikuu vya kilimobiashara cha mipapai na mapapai nchini. visumbufu hivi ni changamoto kubwa kwa kilimobiashara cha zao hili.
Udhibiti wake huhitaji mkulima awe na:
- Nguvukazi (idadi ya wafanyakazi wa shamba) ya kutosha wa kutunza vizuri shamba na kunyunyizia viuatilifu mimea.
- Mtaji (fedha) wa kutosha wa kununulia viuatilifu vya kudhibiti visumbufu hivi kwa kiasi cha kutosha. Ikumbukwe kuwa unyunyiziaji wa viuatilifu ni kwa kila baada ya siku saba (7) wakati wa kipindi cha mvua na kila baada ya siku kumi na nne(14) wakati wa kiangazi. Hairuhusiwi kuruka siku hizo,vinginevyo, mimea itavamiwa na magonjwa na wadudu.
Uwepo wa magugu shambani huchangia kuhifadhi na kuwa mojawapo ya vyanzo vya magonjwa na wadudu waharibifu. Kwa hiyo, ni muhimu, pia, kudhibiti magugu shambani kwa kutumia njia ambazo zimeelezwa kitabuni.
Kitabu hiki ni cha msaada kwa Wakulima,Mameneja wa Mashamba na Wafanyakazi wa mashamba. Kitawasaidia kutambua visumbufu hivi: dalili zake, madhara yanayosababishwa na njia za udhibiti wake.
Pay with DPO