KUTATHMINI MALI NA MAKOSA YA UHARIBIFU WAKE
-
AuthorAl-Muswadiku K. Chamani
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2018
Kitabu hiki kinatumia Sheria za nchi hii na Hukumu za kesi
zilizokwishaamriwa kuwaelimisha wasomaji, hasa, wananchi wa
kawaida na viongozi wao, kuhusu elimu ya Kutathmini Mali ambazo ni
majengo, mazao yaliyo kwenye ardhi, mifugo na maendelezo kwenye
ardhi yenyewe. Kitabu kinaanza kwa kueleza maana ya tathmini na nani
anapaswa kufanya kazi ya kutathmini mali hiyo ili ushahidi wake uweze
kupokelewa mahakamani. Kitabu kinaeleza Sifa za Mtathmini, Vigezo
vya Kutathmini, Utathmini wa Mazao shambani, Tathmini ya thamani
kwa Mdai anayetaka kufidia shamba; Mali iliyokombolea; Utaratibu
wa fidia chini ya Sheria ya Ardhi; Utaratibu wa kuwakilisha tathmini
mahakamani na Hadhi ya ushahidi mtaalamu mahakamani. Aidha, kitabu
kinaeleza juu ya Makosa yanayohusu Uharibifu wa Mali: Dhima ya kosa
la jinai; Matendo ya kuharibu mali; Vipengele vya kuthibitisha kosa;
Ushahidi unaohitajika kuthibitisha kosa; Utetezi katika kosa la kuharibu
mali; Ufafanuzi wa kosa la kuharibu mali katika hukumu; Haki ya mwenye
ardhi kutoa kilichopo kwenye ardhi yake n.k.
Pay with DPO