KILIMO CHA PAMBA TANZANIA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
1. Historia ya pamba nchini
Pamba iliingizwa Tanganyika na Wamisionari na Wafanyabiashara wa
Kijerumani wakati wa utawala wa Wajerumani wa nchi hii katika karne ya
19. Tanganyika ikaanza kupanda pamba (jina sahihi ni mipamba, yaani,
mimea inayozaa pamba) kabla ya mwaka 1900 na ilianza kuuza zao hili
kwenye masoko ya nje mwaka 1920. Uzalishaji wa pamba umeongezeka
haraka tangu 1950.
2. Mazingira ya pamba
Pamba ni zao ambalo hustawi vizuri katika sehemu kubwa ya nchi yetu.
Hustawi katika udongo wa aina mbalimbali mradi tu maji yawe
yanapenya kwa urahisi na usiwe na asidi. Kiasi cha milimita 500 (inchi ishirini)
za mvua hustawisha pamba vema, kama ikinyesha kwa mpangilio
mzuri. Mwinuko wa kuanzia usawa wa bahari hadi mita1,372 (futi
4,500) ndiyo hasa hufaa kwa ustawishaji wa pamba.
Pay with DPO