KILIMO BORA CHA MAHINDI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year1984
Mahindi ni moja ya nafaka muhimu sana duniani na hata katika nchi yetu.
Ni zao ambalo limefanyiwa utafiti kwa undani zaidi katika nchi mbalimbali
duniani, na hasa zile zilizoendelea, kama vile Marekani. Kitabu hiki
kimeandikwa baada ya kupitia baadhi ya maandishi yanayohusu utafiti
huo, hasa ule uliofanyika nchini juu ya zao hili.
Mahindi ni moja ya nafaka ambazo hustawishwa kwa wingi nchini
Tanzania kwenye maeneo yenye mwinuko kati ya mita 0-3,000 kutoka
usawa wa bahari.
Zao hili hustawishwa hasa kwa ajili ya chakula cha wanaadamu na
mifugo. Wakati katika nchi zilizoendelea kilimo cha mahindi ni cha hali
ya juu, hapa nchini bado zao hili linastawishwa hivihivi. Matokeo
yake ni mavuno kidogo ambayo hayalingani na juhudi inayotumika
kulistawisha. Kinachotumika zaidi ni juhudi. Maarifa ya kisasa juu ya
kilimo cha zao hili hayatumiki sana.
Kitabu hiki kinahusu maarifa mapya ya kustawisha zao hili.
Kimeandikwa kwa ajili ya wakulima, wanafunzi na wanavyuo. Nakikabidhi
kitabu hiki kwa watu wote watakaokisoma.
Pay with DPO