Kanuni 13 za Kuzalisha Ngozi Bora
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2015
Tanzania inachukua nafasi ya tatu barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi. Nchi ya kwanza ni Sudani ikifuatiwa na Ethiopia. Kwa sasa nchi hii ina ng’ombe zaidi ya milioni 20, mbuzi zaidi ya milioni 14 na kondoo zaidi ya milioni 4. Kwa viwango vya uvunaji vinavyopendekezwa na serikali vya asilimia 10 – 15 kwa ng’ombe, 28 kwa mbuzi na 29 kwa kondoo kwa mwaka, ngozi zipatazo zaidi ya milioni 3.0 za ng’ombe, milioni 4.0 za mbuzi na milioni 1.1 za kondoo zinategemewa kupatikana kwa mwaka. Ngozi hizi zikiuzwa kwa bei nzuri ni mapato makubwa kwa wafugaji, wafanyabiashara ya ngozi na nchi, zikiuzwa nchi za nje huliingizia taifa fedha za kigeni na kwa viwanda vya ngozi vilivyoko nchini.
Pay with DPO