JUHUDI NA MAARIFA KATIKA KILIMO
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year1980
Kilimo ni sayansi. Kilimo ni kazi ambayo huhusika na viumbe
vyenye uhai na visivyo na uhai. Kutokana na utafiti unaoendeshwa
nchini na katika nchi za nje, kila mwaka kuna njia au mbinu
mpya ambazo hugunduliwa na huweza kuwawezesha wakulima
kujipatia mavuno mengi na yaliyo bora. Maana haja kubwa ya
wakulima na taifa kwa jumla katika kilimo ni kupata mavuno mengi
na yaliyo bora. Kwa upande mwingine, mara nyingi wakulima
huuliza Mabwana na Mabibi shamba, au wao wenyewe huulizana
maswali mbalimbali juu ya kilimo. Kwa bahati mbaya au nzuri
majibu sahihi yanaweza kupatikana au yasipatikane kabisa.
Pay with DPO