Jithibitishie Iwapo Unamiliki Kihalali Ardhi Uliyopewa na Halmashauri za Kijiji naWilaya, Serikali Kuu na Taasisi Nyingine

Jithibitishie Iwapo Unamiliki Kihalali Ardhi Uliyopewa na Halmashauri za Kijiji naWilaya, Serikali Kuu na Taasisi Nyingine

4.0
  • AuthorAl-Muswadiku Chamani
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2023

Jithibitishie Iwapo Unamiliki Kihalali Ardhi Uliyopewa na Halmashauri za Kijiji naWilaya, Serikali Kuu na Taasisi Nyingine.

Ni kitabu kilichoandaliwa na mwandishi (pichani) ambaye ni Mwanasheria, Wakili, Mwalimu na Mwandishi wa vitabu mwenye uzoefu. Kwa kutumia njia ya kuuliza maswali 56 juu ya vipengele vya kumiliki ardhi, amefafanua kwa kina juu ya masuala ya umiliki wa ardhi.

Kwamba, pamekuwepo na migogoro inayoibuka baada ya Halmashauri za Vijiji na Wilaya hata Taasisi mbalimbali zinapogawa ardhi kwa mwombaji wa ardhi. Migogoro hiyo hutokana na baadhi ya watu kudai kuwa, eneo husika ni mali yao. Jambo hili si la kujivunia kwani linaathiri mipango na dhamira kwa wanaohusika. 

Lengo la kitabu hiki ni kutoa tahadhari kwa wahusika kuwa kabla Halmashauri au taasisi husika haijagawa ardhi, basi, huyo mwombaji ahakikishe kuwa, hiyo Halmashauri au taasisi ina umiliki halali wa ardhi hiyo.

Hata hivyo, mnunuzi anaweza kujithibitishia uhalali wa eneo linalohusika alilogawiwa na Halmashauri au Taasisi, alilouziwa, alilorithi, alilopewa zawadi n.k. kwa kusoma kitabu hiki (2022) na kurejea vitabu vifuatavyo: Ufafanuzi wa Sheria ya Kumiliki Ardhi Vijijini Tanzania (2011), Sheria ya Ardhi Tanzania: Umilikaji na Matumizi, (2022) na Kufungua Shauri na Utetezi Mahakamani (2015) vilivyochapishwa na Tanzania Educational Publishers Ltd.

Ni kwa kufanya hivyo, migogoro inayoibuka kutokana kumilikishwa ardhi na vyombo hivyo itapungua.  Sheria na Kanuni zinazohusu umiliki wa ardhi zinamtaka aliyepewa ardhi awe mwangalifu (caveat emptor) ili kupunguza migogoro inayoweza kuibuka hapo baadaye.

Kitabu hiki kinaelezea jinsi Serikali za Mitaa, Serikali Kuu na Taasisi mbalimbali zinavyoweza kumiliki ardhi na utaratibu wa kuigawa au kuitumia.

Pay with DPO

dpo
Book Title Jithibitishie Iwapo Unamiliki Kihalali Ardhi Uliyopewa na Halmashauri za Kijiji naWilaya, Serikali Kuu na Taasisi Nyingine
Author Al-Muswadiku Chamani
ISBN 978-9976-584-27-1
Edition Language
Date Published 2023-12-29
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 103
Chapters 7

Related Books

SHERIA YA ARDHI TANZANIA Umilikaji na Matumizi
SHERIA YA ARDHI TANZANIA Umilikaji na Matumizi
  • SHERIA ZA ARDHI (LAND LAWS)
Tzs5,000.00 Tzs5,000.00
View
Ufafanuzi wa Sheria ya Kumiliki Ardhi Vijijini Tanzania
Ufafanuzi wa Sheria ya Kumiliki Ardhi Vijijini Tanzania
  • SHERIA ZA ARDHI (LAND LAWS)
Tzs5,000.00 Tzs5,000.00
View