JIFUNZE KUSTAWISHA VIAZI VIKUU

JIFUNZE KUSTAWISHA VIAZI VIKUU

4.0
  • AuthorPius B. Ngeze
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year1993

Viazi vikuu ni jina la aina mojawapo ya mazao ambayo
huthamaniwa kwa sababu ya viazi vyake. Kuna aina zaidi ya
600 za viazi vikuu. Lakini, kwa sasa aina maarufu ambazo
hustawishwa kwa wingi duniani hazizidi kumi. Zao hili ni moja
ya mazao maarufu duniani ambayo sehemu inayoliwa hukutwa
ardhini na pengine hewani kwenye mashina. Mazao mengine
maarufu katika jamii hii ya mazao ya mizizi ni viazi vitamu,
viazi mviringo, muhogo, magimbi na mayungwa. Viazi vikuu ni
zao ambalo ni chakula kikuu katika nchi kadhaa za tropiki. Nchi
zinazozalisha viazi vikuu kwa wingi sana duniani ni Malaysia,
Nigeria, Ghana, Kameruni, Benini, Gine, Togo, Amerika ya
Kusini na Vietinamu. Nchi nyingine zilizobaki ambazo zimo katika
ukanda wa tropiki huzalisha zao hili kwa kiasi kidogo na utofautiana
baina ya nchi. Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, kama vile wilaya za
Bukoba, Muleba, Karagwe, Ngara na Biharamulo, nchi za Kenya,
Uganda, Zambia na Angola. Zao hili hupewa majina mbalimbali ya
kiasili kutegemea mahali. Kwa mfano, Wahaya wa mkoa wa Kagera
huita aina iitwayo kwa Kiswahili kiazi kikuu cheupe, Ebilaila na
kiazi kikuu manjano, Kashuli.

Pay with DPO

dpo
Book Title JIFUNZE KUSTAWISHA VIAZI VIKUU
Author Pius B. Ngeze
ISBN 978 9987 426 35 5
Edition Language
Date Published 1992-03-30
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 59
Chapters 7

Related Books

Banana and their Management
Banana and their Management
  • KILIMO CHA MAZAO (MORDEN CROPS HUSBANDRY)
Tzs3,000.00 Tzs3,500.00
View
COTTON IN TANZANIA: Breaking the Jinx
COTTON IN TANZANIA: Breaking the Jinx
  • KILIMO CHA MAZAO (MORDEN CROPS HUSBANDRY)
Tzs3,000.00 Tzs3,500.00
View