Jifunze Kustawisha UYOGA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
Uyoga ni zao la viumbe hai viitwavyo kuvu. Kwa watu wengi
hapa nchini Uyoga unaofahamika ni ule unaookotwa
au unaoonekana ukiota porini au kwenye vichuguu wakati wa
msimu wa mvua. Ukiwaeleza kuwa uyoga hustawishwa kama
ilivyo kwa mazao mengine, hawakuelewi! Ukiwaeleza kuwa
uyoga huweza kumwingizia mkulima fedha nyingi, pia
hawakuelewi.
Lakini, hawana kosa. Kilimo cha Uyoga nchini ni kipya na ni
kichanga. Watu wengi hawajui kuwa uyoga ni zao kama yalivyo
mazao tuliyoyazoea kuyastawisha.
Kwa upande mwingine, nchi yetu inafaa sana kustawisha aina
mbalimbali za uyoga. Uyoga unaostawi nchi zenye baridi na ule
wa nchi za joto unaweza kustawishwa katika maeneo mbalimbali
nchini.
Pay with DPO