Jifunze Kustawisha PARETO
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
Pareto na Alizeti ni mazao mawili ambayo yako katika familia
moja. Pareto ni zao la biashara. Mimea ya pareto hudumu
shambani kwa zaidi ya miaka minne, lakini miaka inayozalisha
kiasi cha maua yenye tija ni mitatu, baada ya hapo paretini
iliyo katika maua huzidi kupungua sana. Kwa sababu hiyo,
mkulima anashauriwa kung’oa mimea yote baada ya mwaka
wa tatu na kupanda zao lingine lisilo pareto.
Umuhimu wa zao hili ni maua yake ambayo yana dutu za
kemikali ziitwazo paretini. Paretini hupatikana baada ya maua
yaliyokauka au yaliyokaushwa kusindikwa kiwandani. Kwa
hiyo, kinachotafutwa katika pareto ni paretini tu.
Pay with DPO