JIFUNZE KUSTAWISHA MTAMA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2004
Mtama ni nafaka muhimu sana katika nchi za tropiki na za tropikiusu.
Ni zao linaloweza kustawi hata katika udongo fukara na hustahimili ukame.
Kati ya aina zote za nafaka, mtama ndio hustahimili zaidi ukame. Mtama una matumizi mengi.
Lakini, hasa hutumika kwa chakula cha binadamu na mifugo, kutengeneza aina mbalimbali za vinywaji na kadhalika.
Kutokana na ustahimilivu wake kwa ukame, serikali nyingi sasa hushawishi wakulima walio katika sehemu
zinazopata mvua chache kuacha kulima mahindi na badala yake wapande mtama. Katika sehemu hizo,
mtama hutoa mavuno mengi kuliko mahindi. Mahindi yanahimizwa yapandwe katika sehemu zenye
mvua za kutosha.Vituo vya Utafiti vya Kilimo vimekuwa vikitafiti aina bora za mtama zinazozaa sana,
ambazo ni kinzani au hazishambu-liwi sana na magonjwa na wadudu waharibifu na ambazo
hazipendwi sana na ndege. Utafiti huo bado unaendelea. Kwa hiyo, ni juu ya wakulima kuitaka
serikali yao kuhakikisha kuwa mbegu bora zaidi zinazopatikana nchini kwa kiasi cha kutosha.
Mabwana shamba wana wajibu wa kuwasaidia wakulima katika jambo hili. Ni juu ya wakulima
kumuuliza Bwana au Bibi shamba wao aina ya mtama iliyo bora zaidi na wapi inapatikana.
Pay with DPO