Jifunze Kustawisha MIMEA YA MATUNDA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
1. Maana ya tunda
Tunda ni zao la mmea linalohifadhi mbegu ambalo hutokana
na ua. Baadhi ya aina za matunda ni chenza, chungwa, embe,
fenesi, bibo, nanazi, ndisi, nyanya, papai, parachichi, peasi,
tikiti, tomoko, tufaha na zabibu.
2. Umuhimu wa matunda
(a) Matunda ni chakula, kwa mfano, ndizi, maboga n.k.
(b) Matunda hutoa kinywaji kisichokuwa na kilevi ndani
yake, kama vile juisi ya machungwa, n.k.
(c) Matunda hutumika kutengenezea pombe na mvinyo yenye
kilevi kwa mfano, zabibu, ndizi n.k.
(d) Matunda ni kiungo, kwa mfano, nyanya.
(e) Matunda yana vii nilishe vinavyohitajika kwa afya yetu.
Matunda mengi yana vitamini C ambayo ni ya lazima
kwa kulinda afya ya miili yetu na sukari ambayo huupa
mwili nguvu.
Pia, matunda yana karotini ambayo baadaye hubadilishwa
na mwili kuwa vitamini A.
Pay with DPO