Jifunze Kustawisha Mikorosho
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2010
Korosho ni moja ya mazao muhimu ya biashara na chakula.
Mikoa inayolistawisha kwa wingi ni Mtwara, Lindi na Pwani.
Pia, hustawi Pemba na Unguja. Soko la korosho ni kubwa nchini
na katika nchi za nje. Tatizo ni kuwa uzalishaji uko chini ya
mahitaji ya soko. Uzalishaji kwa ekari au hektari na kwa mti
mmoja uko chini. Hii inatokana na wakulima wengi kutojua na
kutozingatia kanuni bora za kilimo cha zao hili. Aidha, jitihada
za kufufua na kuboresha mashamba ya mikorosho haziridhishi.
Kitabu hiki ni jitihada ya kueleza kanuni bora hizo kama
mchango wa mwandishi katika kuleta mapinduzi ya kilimo cha
zao hili. Hii ni njia mojawapo ya kutekeleza Kilimo Kwanza
katika Mikoa inayostawisha mikorosho. Kanuni hizo ni hizi
zifuatazo:
Pay with DPO