JASUSI ALIYEMUUA BOSI WAKE

JASUSI ALIYEMUUA BOSI WAKE

4.0
  • AuthorJUSTINE HEZRON BAKE
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2023

Katika hila zao za kutetea haki za wanawake, utadhani si    
haki  za  binadamu,  wanaharakati   wa  Kimagharibi  wanajikuta
wakimtwisha mwanamke wa Kiafrika mzigo mzito wa kusaka noti kama baba, juu
ya mzigo wa kimila wa kulea watoto na kutunzbe walikuwa na ajenda ya siri ya
kuzibomoa familia imara za Kiafrika kwa lengo la kurudisha ukoloni.
Lakini, wanagusa pabaya pale wanapomnasa mke wa Julio na kumjaza ujinga wa
kutelekeza familia ili kuhamia mitaani kwa kisingizio cha kufanya ujasiriamali;
wakimrubuni kwa vijisenti vya mikopo ya kuwakomboa wanawake kutoka kwenye
mamlaka ya waume zao, au mfumo dume, kama wanavyouita! Na hicho ndicho
kilichowaponza wahalifu waliojipatia mamilioni ya fedha kwa kuendesha shirika
binafsi la kijasusi likitumia TEHAMA na maafisa wastaafu wa jeshi la polsi na jeshi
la wananchi kuwanasa wake za watu waliowasaliti na kuwachukua video za matusi
yao.
Katika sakata la Julio kumkomboa mke wake, majasusi hawa pamoja na washirika
wao wanajikuta wakipukutika kama kumbikumbi walipojaribu kutoroka kutoka
kwenye pango la jumba lao la kifahari lililosetirika katikati ya msitu wa majanga wa
Mabwepande, Dar es Salaam, Tanzania. Kila aliyechomoka alikutana na mtutu
kabambe wa bastola ya mdunguaji sugu wa kike, Zuhura, au Kimbunga Katalina
kwa rakabu yake.
Ili kufahamu kiundani yaliyojiri msituni humo, katika pambano la Julio kumkomboa
mke wake; na kupelekea kukomeshwa kwa ufeministi wa kibeberu nchini humo,
soma mwanzo mpaka mwisho mwa riwaya hii ya kibabe. Furahia!

Pay with DPO

dpo
Book Title JASUSI ALIYEMUUA BOSI WAKE
Author JUSTINE HEZRON BAKE
ISBN 978-9976-584-01-1
Edition Language Kiswahili
Date Published 2023-11-30
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 110
Chapters 9

Related Books

Penzi liliponzwa
Penzi liliponzwa
  • RIWAYA
Tzs5,000.00 Tzs7,000.00
View
Rita Koku
Rita Koku
  • RIWAYA
Tzs5,000.00 Tzs7,000.00
View