Wanyonge Wasinyongwe
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2008
Sheria iliyopo ambayo ilitungwa wakati wa ukoloni hairuhusu matumizi ya vyombo vya usafiri vyenye magurudumu mawili, yaani, pikipiki na baiskeli, kubeba abiria kwa kuwatoza nauli, lakini inaruhusu kubeba abiria mradi usiwatoze nauli! Tangu Uhuru, sasa ni zaidi ya miaka 47, mambo mengi yamebadilika katika kipindi hicho. Mojawapo ni ongezeko la watu kutoka milioni tisa (9) mwaka 1961 na kufikia watu wapatao milioni arobaini (40) kwa sasa. Mahitaji ya usafirishaji wa wananchi yamebadilika sana. Eneo moja ambalo kuna mabadiliko ni ongezeko la baiskeli na pikipiki nchini na matumizi yake kibiashara kwa kubeba abiria na kuwatoza nauli ndogo. Biashara hii imefumuka katika majiji, manispaa, miji, mitaa, vijiji na vitongoji vya nchi nzima. Niambie ni wapi biashara hii haipo?
Pay with DPO