SILAHA 100 ZA KIONGOZI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2008
Kiongozi ni mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, mwenye madaraka au mamlaka juu ya mtu mmoja au watu wengi. Maana nyingine ya Kiongozi ni mtu aliyepewa jukumu la kuongoza mtu mmoja au watu wengi. Mtu mmoja huyo anaweza akawa mwanandoa mwenzie au mtu mmoja mwingine ambaye ana ushirika naye. “Watu wengi” wanaweza kuanzia wanafamilia yake hadi taifa zima. Kwa upande mwingine, uongozi ni mamlaka ya kuongoza mtu mmoja au watu wengi kwa lengo maalumu. Lengo hilo linaweza kuwa ni la maendeleo au ukombozi wa aina fulani kwa mtu au watu hao. Uongozi katika jamii yoyote ni wa lazima. Pakiishakuwapo watu wawili lazima mmojawapo awe kiongozi, vinginevyo hapatakuwepo amani wala maendeleo. Hata kwa baadhi ya aina ya wanyama, upo utaratibu au mfumo wa kuwa na viongozi katika makundi au katika vitendo vyao.
Pay with DPO