Uhusiano wa Chama Tawala, Serikali na Sheria za Nchi
-
AuthorAl-Muswadiku K. Chamani
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2018
Vyama vya siasa duniani kote vina lengo kuu moja, nalo ni kugombea na kushindana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na Chaguzi Ndogo ili kushinda na kushika dola kwa kuunda serikali kuu na serikali za mitaa. Kwa sababu hii, katika madhumuni mengi ya chama cha siasa chochote, dhumuni namba moja ni kushika dola. Kwa Tanzania, lengo ni kushika dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na dola ya Zanzibar. Chama cha siasa kina Sera na misimamo fulani maalumu ambayo hukitofautisha na vyama vingine vya siasa. Wakati wa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu, Chama cha siasa hutumia Sera na misimamo yake hiyo kuandaa Ilani ya Uchaguzi huo. Ilani hiyo ni Ahadi za Chama hicho kwa wananchi wote (watakaopiga kura na ambao hawatapiga kura) kuwa wakikichagua kitaunda serikali ya kuzitekeleza kupitia kuandaa sera, na kutokana na sera hizo kuandaa miswada ambayo itapelekwa Bungeni na kupitishwa kuwa sheria.
Pay with DPO