Ufugaji Bora wa Kuku
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2008
Ndege maarufu wanaofugwa na binadamu kwa ajili ya mayai na nyama yao ni wa aina sita zifuatazo: kuku, bata, batamzinga, bata bukini, njiwa na kanga. Kati ya hao sita, ndege aliye maarufu zaidi ya wengine ni kuku. Kutokana na umaarufu huo, kitabu hiki kinahusu ndege huyu. Kuku wanaofugwa hapa nchini hutengwa katika aina kuu mbili: (a) Kuku wa Kienyeji na (b) Kuku wa Kigeni. Kuku wa Kigeni nao hutengwa katika aina kuu mbili, yaani (a) Kuku Kizazi Menyu na (b) Kuku chotara. Hapa nchini kuku wanaofugwa zaidi ni Kuku wa kienyeji na Kuku chotara. Kuku chotara ni kwa ajili ya ufugaji wa kibiashara. Kuku Kizazi Menyu hawafugwi.
Pay with DPO