Uboreshaji wa Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
-
AuthorSamson Malimi Sabbo
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2015
Uboreshaji wa Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni kazi inayohitaji maarifa na juhudi ili kupata mazao mazuri na bora. Wanunuzi wa kuku hupendelea kuku bora, mayai bora, nyama bora ambayo hupatikana kutokana na juhudi ya mfugaji kuweza kuwatunza kuku wake ipasavyo. Ufugaji bora wa kuku humhitaji mfugaji kuelewa na kuzingatia kanuni za ufugaji bora wa kuku, ambao ni pamoja na ujenzi wa banda bora; uchaguzi sahihi wa njia za ufugaji; utengenezaji na ulishaji wa chakula bora, udhibiti wa magonjwa; uzalishaji wa koo bora na elimu ya masoko. Ni lazima mfugaji wa kuku wa kienyeji awe na elimu hii ili aweze kuendesha shughuli zake kwa usahihi na kwa manufaa ya wote wale watakaopata huduma kwake.
Pay with DPO