Mwanzo na Mwisho wa Uongozi wa Kisiasa

Mwanzo na Mwisho wa Uongozi wa Kisiasa

4.0
  • AuthorPius B. Ngeze
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2008

Safari ndefu huanza na hatua moja. Safari yangu ya uongozi wa kisiasa ilianza tarehe 10 Aprili, 1974, nilipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tawi la TANU, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa . Wakati huo nilikuwa Ofisa Mipango wa Wilaya hiyo. Mwaka uliofuata, 1975, nilipandishwa cheo kwa kuteuliwa na Rais kuwa Kamishna Msaidizi wa Idara ya Mipango na Usimamizi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais. Nikahama Iringa na kwenda kuishi Dodoma. Huko nikachaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi la TANU la Ofisi hiyo. Mwaka 1977 nikachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera kwa vipindi vinne mfululizo (1977-82, 1982-1987, 1987 - 1992 na 1992 - 1997) na kipindi kimoja cha 2002 -2007. Kutokana na kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa unakuwa moja kwa moja Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa. Baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara, 1995, mwaka uliofuata nilihamia huko kutoka Bukoba. Kutokana na ugumu wa kuwa Mwenyekiti wa Mkoa huku ukiwa Mbunge na nikiishi Rulenge, Wilayani Ngara, nikaamua kutogombea Uenyekiti wa CCM wa Mkoa mwaka 1997. Nikaaga bila kufikiria kuwa ningeweza kurudi tena kugombea na kuchaguliwa.

Pay with DPO

dpo
Book Title Mwanzo na Mwisho wa Uongozi wa Kisiasa
Author Pius B. Ngeze
ISBN 978-9987-07-010-7
Edition Language KISWAHILI
Date Published 2008-05-09
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 52
Chapters 8

Related Books

SILAHA 100 ZA KIONGOZI
SILAHA 100 ZA KIONGOZI
  • UONGOZI NA UTAWALA (LEADERSHIP & ADMINISTRATION)
Tzs5,000.00 Tzs6,000.00
View
Kudos President  Magufuli
Kudos President Magufuli
  • UONGOZI NA UTAWALA (LEADERSHIP & ADMINISTRATION)
Tzs5,000.00 Tzs6,000.00
View