Heko Rais Magufuli

Heko Rais Magufuli

4.0
  • AuthorNkwazi Nkuzi Mhango
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2018

Kimsingi, kitabu hiki ni kama “barua ya wazi” kwa watu wote, kuhusu Rais John Pombe Magufuli, ambayo kwayo mtunzi wake Ndugu Nkwazi Mhango, ameweka bayana rai za kutoka ndani ya moyo wake, akieleza ni jinsi gani anavyoridhishwa na kazi za uongozi anazofanya Mheshimiwa Magufuli, Rais wa awamu ya tano ya uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini, sambamba na hilo, mwandishi huyu pia ametoa ushauri wake binafsi kwa Rais, kuhusu mambo yale ambayo yeye anaona kuwa yanafaa kwa Rais kuyafanya, au kuepuka kuyafanya. Kinachopendeza zaidi, ni kwamba mwandishi ametoa mawazo yake hayo kwa njia ya kuvutia sana, alipotumia staili ya uandishi wa tenzi au shairi, ambayo kwa hakika imeongeza utamu na kusababisha raha zaidi kwa msomaji. Nionavyo mimi, mawazo yake yanaendana vizuri na mawazo ya Watanzania walio wengi, ambao wanamuona Rais Magufuli kama “Nyerere wa kizazi cha sasa”; hasa, kuhusiana na ubunifu wake, pamoja na shauku yake katika kutelekeza miradi ile ambayo awali ilibuniwa na kuasisiwa na Mwalimu Nyerere, lakini, hakuweza kuitekeleza kutokana na mazingira yaliyokuwapo katika kipindi husika, yakiwa nje kabisa ya uwezo wa Mwalimu Nyerere kuyarekebisha. Miongoni mwa miradi hiyo, ni mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge, na ule wa kuhamishia Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Pay with DPO

dpo
Book Title Heko Rais Magufuli
Author Nkwazi Nkuzi Mhango
ISBN 978 9987 07 091 6
Edition Language KISWAHILI
Date Published 2018-01-01
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 136
Chapters 13

Related Books

SILAHA 100 ZA KIONGOZI
SILAHA 100 ZA KIONGOZI
  • UONGOZI NA UTAWALA (LEADERSHIP & ADMINISTRATION)
Tzs5,000.00 Tzs6,000.00
View
Kudos President  Magufuli
Kudos President Magufuli
  • UONGOZI NA UTAWALA (LEADERSHIP & ADMINISTRATION)
Tzs5,000.00 Tzs6,000.00
View