Kabaka mwanga na Wafia dini ya Kikristo, Uganda
-
AuthorAhmad Mujaki
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2019
Tamthilia hii ina mwelekeo wa habari zinazomhusu Kabaka Mwanga II, ambaye alikuwa Kiongozi Mkuu wa Buganda, nchini Uganda. anakumbukwa sana kwa ajili ya maelekezo aliyoyatoa ya kuwatesa na kuwaua waamini wapya na wa kwanza wa dini ya kikristo (wakatoliki 22 na Wanglikana 23) nchini Uganda, kati ya tarehe 31 januari 1885 na 27 Januari 1887. kwa taeatibu za dhehebu la katoliki, wale wafia dini 22, sasa ni Watakatifu.
Hata hivyo, kama utakavyosoma katika tamthilia hii iliyofanyiwa uchunguzi wa kina, Kabaka Mwanga II, alifanya mengi zaidi ya hayo.
Katika tamthilia hii, kuna mchanganyiko wa habari za kubuniwa ambazo zinafikiriwa kuwa kweli, japokuwa zinaweza kuwa za kubuni tu kwa namna fulani, sambamba na habari za matukio ya kweli, ili kukupatia wewe msomaji kitu kinachoweza kukiita burudani ya kisiasa na jamii.
Karibu kwenye tamthilia hii.
Pay with DPO