Haki za Madereva, Abiria na Polisi Barabarani

Haki za Madereva, Abiria na Polisi Barabarani

4.0
  • AuthorAl-Muswadiku K. Chamani
  • PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
  • Year2013

Awali nilipata kumfahamu mwandishi wa kitabu hiki baada ya kusoma baadhi ya vitabu vyake, vikiwamo, Sheria ya Ardhi Tanzania: Umilikaji na Matumizi, Fahamu kisheria Ofisa Mtendaji wa Kata nchini Tanzania, Ufafanuzi wa Sheria ya KUmiliki Ardhi Vijijini Tanzania, Haki zangu Mbele ya Polisi, Haki za Mwalimu Tanzania na Uwakilishi Mahakamani Tanzania. Hatimaye nimemfahamu zaidi baada ya kukutana naye ana kwa ana Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba, katika kazi yake ya Uwakili wa kujitegemea akitetea raia katika mashauri mbalimbali. Ni vyema niseme wazi kuwa lengo la mwandishi wa vitabu hivi limekuwa mchango mkubwa kwa jamii yetu na hasa katika kipindi hiki ambapo nchi yetu ipo kwenye mfumo wa vyama vingi. Mfumo huu unatoa nafasi kwa jamii kutafuta na kujua haki na stahili za kisheria za kila mwanajamii. Zipo njia nyingi za mtu kujua haki na stahili zake za kisheria. Njia mojawapo ni kusoma vitabu mbalimbali vya sheria vinavyohusu haki hizo. Kwa mwandishi kutumia njia ya maswali na majibu amerahisisha njia ya kumwezesha mwananchi wa kawaida kuelewa au kupata ujumbe, kwani ni maswali yanayotokana na hali halisi iliyopo katika jamii yetu.

Pay with DPO

dpo
Book Title Haki za Madereva, Abiria na Polisi Barabarani
Author Al-Muswadiku K. Chamani
ISBN 978 9987 07 048 0
Edition Language KISWAHILI
Date Published 2013-05-27
Publisher Tanzania Educational Publishers Ltd
Pages 95
Chapters 50

Related Books

Usalama Barabarani Jukumu Letu
Usalama Barabarani Jukumu Letu
  • USALAMA BARABARANI (SAFETY ON ROADS)
Tzs5,000.00 Tzs5,500.00
View