Changamoto za Maendeleo ya Mkoa wa Kagera
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2014
Baadhi ya watu, wakiwamo marafiki zangu, walinishangaa kuacha utumishi wa serikali, ambao ulionyesha matumaini makubwa kwa kupanda ngazi harakaharaka katika utumishi wa umma na kujitumbukiza katika siasa! Nikawajibu kwamba, najaribu, nikishindwa kuchaguliwa, nitarudi serikalini, nikishinda, ningependa kuwatumikia wananchi wa mkoa wangu, wakati huo ukiitwa Mkoa wa Ziwa Magharibi. Niliposhinda, nikahamia Bukoba kutoka Dodoma na kazi ikaanza. Mkoa ulivyokuwa mwaka 1977 Wakati huo wananchi wengi wazaliwa wa mkoa huu waliogopa kuhamia na kufanyia kazi katika mkoa huu. Walihusisha mkoa huu na majungu, tabia ya kushtakiana na shida ya usafiri, hasa, baada ya kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki. Aidha, palikuwapo tatizo la kubaguana na kudharauriana baina ya Wahaya na Wahaya na Wahaya na makabila mengine ya mkoa huu, hasa, Wanyambo,Wahangaza na Washubi wa Ngara na Wasubi wa Biharamlo. Palikuwapo pia, migogoro ya kidini, hasa ndani ya madhehebu ya Kii slamu. Palikuwapo migogoro ya kisiasa baina ya wanasiasa wa ngazi za Wilaya, Kata na hadi Vijijini. Wakati fulani palionekana kuwapo ukuta kati ya wanasiasa na maofisa wa serikali, lakini, Chama kilikuwa kimeshika hatamu za uongozi. Palikuwapo baadhi ya watu kujiona ni bora kuliko wengine. Kiuchumi mkoa huu ulikuwa nyuma sana. Hivyo ndivyo nilivyoukuta mkoa na hapo ndipo palikuwa pa kuanzia kazi.
Pay with DPO