MWONGOZO WA KUANDIKA HADITHI FUPI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2026
Mwongozo wa Kuandika Hadithi Fupi ni kitabu cha kipekee kilichoandikwa kwa ajili ya waandishi wanaoanza kuandika hadithi hadi wenye uzoefu. Kinaelezea hatua kwa hatua jinsi ya kuunda hadithi fupi zenye msukumo, wahusika thabiti, taswira halisi na matukio yanayoshika hisia za msomaji.
Kitabu hiki kinatoa:
• Mbinu za uandishi na uhariri wa hadithi fupi
•Mifano halisi ya hadithi fupi za aina mbalimbali zenye: ucheshi, kihistoria, kijamii, hisia na kidijitali
•Mikakati ya kuwasilisha na kuchapisha hadithi, kiasili na kidijitali.
Ni mwongozo kamili kwa:
•Wanafunzi wa fasihi
•Waandishi chipukizi na wenye uzoefu
•Waalimu, warsha za fasihi na mashirika ya kitamaduni
•Kwa yeyote anayetaka kuboresha uandishi wake wa Kiswahili na kufanikisha hadithi fupi zenye thamani ya kijamii na kisanii
Kitabu hiki kinatoa elimu kwa waandishi ili kuandika hadithi fupi kwa wingi maana hadithi hazichapishwi tu, zinaishi,
zinaelimisha na kushika hisia za wasomaji.
Pay with DPO

