JOHN POMBE MAGUFULI Miaka 5 ya Hapa Kazi Tu, Nidhamu Kazini, Vita dhidi ya Rushwa, Uongozi Mkali Usio na Mizaha, na Mwasisi wa Miradi 12 ya Kimkakati Iliyopandisha Kileleni Uchumi wa Taifa
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2026
Kitabu hiki kimeandikwa kama kumbukumbu ya kitaifa, tathmini ya uongozi na sombo la maarifa kwa vizazi vya sasa na vijavyo kuhusu kipindi cha miaka mitano cha uongozi wa John Pombe Magufuli, aliyeliongoza Taifa la Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 kwa falsafa iliyotikisa misingi ya utawala wa umma: “Hapa ni Kazi Tu.” Katika historia ya Tanzania ni viongozi wachache walioweza kubadilisha mienendo ya utendaji kazi wa Serikali, mtazamo wa wananchi kuhusu mali ya umma na ujasiri wa Taifa katika kusimamia rasilimali zake kwa kasi, uthubutu na msimamo thabiti kama alivyofanya Rais Magufuli. Kipindi chake cha uongozi kilijengwa juu ya nidhamu kazini, uwajibikaji wa moja kwa moja, vita dhidi ya rushwa na msimamo mkali dhidi ya uzembe, ufujaji na mizaha isiyo na tija katika utumishi wa umma. Aidha, Kitabu hiki kimepangwa katika sura 20, zikianza na wasifu wa Rais Magufuli, kuingia kwake madarakani, falsafa ya Hapa ni Kazi Tu, vita dhidi ya rushwa, mtindo wake wa uongozi mkali, uasisi wa miradi 8 ya kimkakati hadi tathmini ya jumla na urithi wake katika historia ya Tanzania. Ni vyema kitabu hiki kisomwe na Watanzania wote.
Pay with DPO

