JIKO LA UKOMBOZI
-
AuthorEsther Evarist Nyawale
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2026
Mwandishi wa kitabu hiki, Jiko la Ukombozi (Tamthiliya ya Runinga), Esther Evarist Nyawale ni Mwanamke kijana na mwandishi wa kazi bunifu kutoka mkoani Morogoro nchini Tanzania. Mwandishi amesajiliwa na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kama Mwandishi wa Miswada ya Filamu na Mwongozaji wa Filamu. Mwaka 2026 mwandishi aliweza kushinda Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, nyanja ya Tamthiliya, kama Mshindi wa Tatu katika nyanja hii kupitia kitabu hiki. Tuzo hii hutolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia taasisi yake iitwayo Taasisi ya Elimu Tanzania. Kitabu hiki kinaelezea jinsi Jiko linavyoweza kuleta na kuimarisha Ustawi wa Chakula kwenye jamii. Falsafa ya mwandishi ni kuzungumza na jamii kuwa biashara si tu zile za kufanya uchuuzi kutoka mataifa ya magharibi na mashariki na kuzileta Tanzania na Afrika, bali pia zipo biashara kama mifumo ya jikoni, vyakula asilia, michezo, muziki, fasihi, utalii na filamu zetu kutoka hapa Tanzania na barani Afrika ambazo tunaweza kuzifanya ili kusaidia jamii zetu, lakini, pia kuzipeleka biashara hizo kimataifa. Ili kuendeleza jukumu hili kwa vitendo, mwandishi ameweza kujiunga na Mfumo wa Taasisi ya Confucius iliyo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako anaendelea na mafunzo ya Lugha ya Kichina. Mwandishi haishii tu kujifunza lugha hii bali pia kujifunza Tamaduni za Kichina kupitia Filamu ili kupata uelewa na uwezo wa uandishi wa miswada ya filamu pamoja na kujenga uhusiano kati ya Filamu za Kiswahili na Kichina; hasa zinazohusu biashara, lugha zetu, vyakula, muziki, mitindo ya maisha, elimu, fasihi na utalii.
Pay with DPO

