JIFUNZE KUSTAWISHA MBOGA

Lengo la kitabu hiki ni kuwa mwongozo kwa wadau mbalimbali,
wakiwamo wakulima wa mazao ya mboga,

By PIUS B. NGEZE

Kitabu hiki kimeandikwa ili kiwasaidie Wakulima kuendeleza aina
mpya ya kilimo, yaani, Ustawishaji wa Mboga. Kutokana na wingi wa
aina za mboga zilizopo, kimeandikwa kwa muhtasari. Hata hivyo,
hatukuweza kueleza kilimo cha aina zote za mboga. Zipo chache ambazo
zimeachwa.
Kitabu kimegawanywa katika sehemu mbili: Sehemu ya Kwanza inaelezea
Misingi ya Kustawisha Mboga, Sehemu ya Pili inaelezea Ustawishaji wa
aina mbalimbali za Mboga. Kila sehemu imegawanywa katika sura
kadhaa. Sehemu ya Kwanza ina sura kumi na moja (11) Sehemu ya Pili
ina sura sita (6). Mwishoni mwa kila sura yapo Maswali ya kumsaidia
msomaji ajipime kama ameielewa vizuri sura hiyo. Mwishoni kabisa ya
kitabu, zipo Nyongeza tatu (3), Tafsiri na Marejeo.

Mboga ni mmea au sehemu yoyote ya mmea inayoweza kuliwa na binadamu ambayo haina sukari kama matunda. Mboga huweza kuliwa zikiwa zimepikwa na mara nyingi huwekewa chumvi ili kuongeza ladha na pia huweza kuliwa zikiwa mbichi kwa mfano kwenye kachumbari. Mboga ni sehemu muhimu sana katika mlo uliokamilika, hii imesababisha ukuaji wa kasi wa soko la mboga na upandaji wa mboga katika maeneo mengi ya mijini na vijijini.

Changamoto za kilimo cha mboga

Nchi hii ina hali ya hewa na mazingira mazuri kwa kustawisha aina
mbalimbali za mboga (na matunda) mwaka mzima. Mazao hayo ni kwa
ajili ya chakula bora na biashara. Virutubisho vilivyo katika mazao hayo
ni muhimu kwa afya nzuri za watu. Hata hivyo, kilimo cha aina hii
kinakabiliwa na changamoto zifuatazo:
(a) Wakulima kutumia teknolojia duni za uzalishaji zinazosababisha
mavuno kidogo na yenye ubora hafifu.
(b) Uvunaji usiozingatia viwango unaotokana na matumizi ya vifaa duni.
(c) Kutofanya uchambuzi wa kutenganisha mazao bora na yale yenye
magonjwa, kasoro na ubora duni.
(e) Ukosefu wa uangalifu wakati wa uvunaji ambapo mazao hudondoshwa,
hupwa chini, na hufungashwa bila ya kuchambuliwa vizuri. Matokeo
yake ni kusababisha mazao hayo kuchubuka, kupasuka, kuoza
na kuongeza kasi ya upotevu wa mazao hayo.
(f) Kutokana na miundombinu dhaifu na ufungashaji duni wakati wa
usafirishaji mazao huchubuka, hupasuka, hubonyea na husagika.
Kutokana na changamoto hizo, mazao ya mboga hayakidhi viwango
vinavyotakiwa na soko linalohitaji mboga zilizo bora na salama.

P17TEPU19
P17TEPU19
P17TEPU19

Lengo la kitabu hiki ni kuwa mwongozo kwa wadau mbalimbali,
wakiwamo wakulima wa mazao ya mboga, kuhusu:
(i) Kanuni bora za kilimo cha mazao ya mboga, yaani, matumizi ya
teknolojia za kisasa.
(ii) Njia bora za uvunaji wa aina mbalimbali za mboga.
(iii) Njia bora za fungashaji wa mboga.
(iv) Njia bora za usafirishaji wa mboga
(v) Kuhifadhi mazingira na viumbe wengine wakati wa kuendesha kilimo
cha mboga. Hii ni pamoja na:
• Kutochafua vyanzo vya maji.
• Matumizi bora ya maji.
• Matumizi bora ya pembejeo za kilimo, hasa mbolea za viwandani
na viuatilifu
• Ulinzi wa bayoanuai.

BEI YA KITABU HIKI:

Soft copy ni 5,000/-
Hard copy ni 15,000/-

UPATIKANAJI WA KITABU HIKI

Kwa kupakua nakala ya softcopy katika Website yetu ya
https://tepu.co.tz/index.p…/…/jifunze-kustawisha-mbogamboga/

Au
Tanzania Educational Publishers Ltd,
Barabara ya Uganda,
Kiwanja Na. 45, Kitalu MDA,
Simu: 0685 997583 / 0758 147871
Baruapepe: tepultd@yahoo.com
Tovuti: www.tepu.co.tz,
S.L.P. 1222,
Bukoba, Tanzania.

Spread the word


Facebook-f


Twitter


Google-plus-g


Linkedin-in


Snapchat

Loading...