USHIRIKA TANZANIA
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year1975
Shabaha kuu ya Vyama vya Ushirika vilipoanzishwa, ilikuwa kuuza
mazao ya wanachama kwa bei nzuri na wakati huohuo kuondoa unyonyaji
wa wafanyabiashara ambao walikuwa wakinunua mazao hayo kwa bei ya
chini na kuyauza kwa bei ya juu. Katika kufanya kazi hiyo, hasa baada ya
kupata uhuru wetu, vyama hivyo vimekumbana na matatizo mbalimbali
ya kukua. Lakini, kwa ushirikiano baina ya TANU, serikali, wanachama
na viongozi wa vyama hivyo matatizo hayo yalipungua.
Kazi mojawapo iliyofanywa na TANU ilipoanzishwa ilikuwa kuhimiza
uanzishaji na uendeshaji bora wa vyama vya ushirika hasa katika zile
sehemu za nchi hii ambazo hazikuwa na vyama hivyo. Vilevile kuimarisha
vyama hivyo katika sehemu ambazo zilikuwa navyo tayari. Maendeleo ya
vyama vya ushirika tangu mwaka 1954, TANU ilipozaliwa, na hasa baada
ya kupata Uhuru, ni uthibitisho maalumu unaonyesha jinsi wananchi
walivyoitikia wito wa TANU wa kuanzisha, kuendesha vizuri na kuimarisha
vyama vya ushirika nchini.
Pay with DPO