KILIMO CHA UMWAGILIAJI
-
AuthorPius B. Ngeze
- PublisherTanzania Educational Publishers Ltd
- Year2008
Mwaka 1974 kulitokea upungufu wa mazao muhimu ya chakula
nchini. Upungufu huu ulitokea kwa sababu ya ukosefu wa mvua
katika mikoa kadhaa katika msimu wa kilimo wa 1972/73 na
hata msimu wa kilimo wa 1973/74. Taifa lililazimika kuagiza
mahindi, mchele na ngano kutoka nchi za nje kwa thamani ya
shilingi milioni 935 (za wakati huo).
Nafaka hizi zilikuwa za kutosheleza mahitaji ya wananchi hadi
Septemba, 1975. Ukame huu pia ulisababisha malisho ya mifugo
kukauka na kiasi cha mifugo kufa katika mikoa fulani.
Pay with DPO